*Nukuu 12.kutoka kwenye kitabu kipya cha Fahamu ya Ndoa Kabla ya Ndoa*

1. Mzazi mwenye hekima huwasimulia watoto wake makosa aliyofanya ili wasiyarudie; mzazi wa ajabu anawaambia watoto wake kueni myaone!

2. Zamani walichunguzana kabla ya kuona ndoa zikadumu; siku hizi wanachunguzana baada ya kuona ndiyo maana ndoa hazidumu

3. Mtoto wetu akikushinda turudishie, usimuue. Mbona sisi hatukumuua? Vile vile mumeo akikushinda usimkate sehemu za siri, muombe talaka urudi nyumbani.  

4. Ndoa za siku hizi mume akifilisika mke anamkimbia; mume akifanikiwa anakimbia mke!

5. Maisha ni mgogoro ndiyo maana mwisho wake ni kifo!

6. Usitegemee makubwa sana kwenye ndoa, mapenzi ni yale yale na watu ni wale wale wametofautiana aina za matatizo tu.

7. Ukiishaoa unatakiwa kuishi kama baba na siyo mvulana.Ukiishaolewa unatakiwa kuishi kama mama na siyo binti. Hata mavazi yenu lazima yabadilike. Uko tayari?

8. Usiingie kwenye ndoa kwa sababu ya msukumo wa hisia za kimwili. Usiingie kwenye ndoa kwa sababu ya mimba. Usiingie kwenye  ndoa kwa sababu ya msukumo wa wazazi. Usiingie kwenye ndoa kwa sababu ya msukumo wa marafiki

9. Ndoa ina vyote. Vitamu na vichungu! Inaitwa chungu tamu. Uhuru ni wako. Ukitaka kuutafuta utamu utaupata,ukitaka uchungu pia utaupata wa kutosha!

10. Ndoa hujengwa kwa mawe ya upendo na sakafu ya utii!

11. Kwenye Ndoa Hakuna Simu Yetu, Kuna Gari Letu, Nyumba Yetu, Watoto Wetu

12. Uwe umeolewa ama umeoa utatongozwa tu. Mwanamke utatongozwa ili wakule, mwanaume utatongozwa ili wakuchune.

Karibu katika Jukwaa la Fikra,  app yako pendwa kabisa.

Wako Dady Lutelemla katika ujenzi wa fikra huru napatikana kwa WhatsApp namba 0620306815.