Katika maisha kuna changamoto nyingi sana ambazo zinaweza kukukwamisha kufikia malengo yako ya kibiashara, unapanga kuanzisha biashara lakini kwa muda mrefu umekuwa ukiwaza na kupanga mipango ambayo mwisho wa siku matekeo hauyaoni.
Miaka inakatika, umri unasogea, akili nayo inachoka. Biashara ni kitu ambacho kinahitaji kujitoa kwa namna yoyote na kwa hali yoyote ulitokuwa nayo kwa muda fulani. Kuanzisha biashara hakuhitaji kitu kikibwa ila kunahitaji akili kubwa sana.
Kama una msukukimo unakusukima kufanya biashara na hauna kitu, angalia kitu ulichoshikilia mkononi mwako, inaweza ikawa simu, rasilimali yoyote, na hata watu wanaokuzunguka.
Bahati nzuri dunia inavyoenda kwa sasa unaweza kuanzisha biashara kwa kuuza kile usichokizalisha, kuuza hata kama usipokuwa na sehemu maalumu ya kuweka biashara hiyo!
Kitu pekee ninchotaka kukushauri wewe msomaji wa jukwaa la fikra ni kwamba, hakuna hatua kubwa yoyote iliyofikiwa na mtu yeyote aliyefanikiwa pasipo kuanza na kidogo!
Anza kidogo, weka nidhamu, weka juhudi, weka malengo! Anza kwa kufikiria miaka kumi ijayo, panda mbegu, mwagilia mpaka ichipue, ilinde kwa muda wote.
Kitu pekee kinachotufelisha tuliowengi ni kuanza leo unataka ufanikiwe kesho! Achana na hayo mawazo! Anza kidogo kwa kile kilicho mkononi mwako!
Jukwaa biashara na Dady Lutelemla
Napatikana whatsap kwa +255620306815

0 Comments