Siri ni maisha mwanangu, huna siri huna maisha. Mwanangu jaribu kuwa kama watu waliofanikiwa, mtu aliyefanikiwa utashangaa tu ameoa, utashangaa tu ameolewa, utashangaa tu ana nyumba, utashangaa tu amejifungua mtoto, huwa hawatangazi.
Mwanangu ukiweza kujificha adui asikuone ila wewe ukamuona jua ushindi ni wako hata kama una silaha dhaifu, kujificha ni moja ya kanuni za ushindi. Mwanangu watu wengi waliofeli huwa hawana siri, wakipatwa jambo wanawashwa, wakipata safari wanaaga aga mpaka safari inaahirishwa, wakopata kiwanja wanakimbilia kuombewa hadi kiwanja hakinunuliki.
Hakuna siri ya watu wawili mwanangu, siri ni ya mtu moja, siri ya wengi siyo siri tena huo ni mkutano. Siri ni ushindi mwanangu na ushindi huwa ni wa mtu moja.
Kile asichokijua adua yako ndiyo salama yako
Siri ni ulinzi, jilinde, mtu asiyekuwa na siri hana ulinzi. Kazi ya siri ni kuweka mambo sawa.
Mwanangu ili ufanikiwe ni lazima ujue siri fulani fulani na ukizijua ficha. Watu waliofanikiwa wanatumia akili, nguvu na mali ili siri zisifichuke.
Matajiri wengi hawasemi siri za utajiri wao zaidi ya kukwambia FANYA KAZI. Watu waliofanikiwa kwenye nmahusiano hawasemi siri zao zaidi ya kukusihi upendo! Kuna siri mwanangu!
Nimemwachia mtandao ujumbe huu ili ukirudi akupatie, na ukiupata nipigie simu yangu +255620306815.
Tunza siri mwanangu!

0 Comments