Hakika hakuna mtu anayeishi bila kuwaza biashara, haijarishi mtu ana hali gani ya kimaisha ila linapokuja suala la biashara kichwa huwa kila moja kizunguka kimawazo.

Mtu huwaza aanzishe biashara gani, afanye kitu gani kitakachomuingizia pesa, kitakachompa heshima katika jamii inayomzunguka. Hakika hakuna mtu asiyewaza hayo.

Hapo zamani za kale biashara ilitatua matatizo ya kijamii kwa kubadilishana bidhaa kwa bidhaa, yaani mtu aliyekuwa na mahitaji juu ya kitu fulani alitakiwa kumfuata mwenye uhitaji wa kitu tofauti na anachomiliki mwenzake, maisha yalinoga sana.

Dunia imekuwa na changamoto nyingi sana na njia pekee ya kuzitatua changamoto hizo ni kufanya biashara. Kuna watu wapo wanaombea mtu augue ili afanye biashara yake ya kuuza dawa.

Kuna mtu anaombea mtu afe ili afanye biashara yake ya kuuza majeneza, zote hizo ni biashara na zinategemea fursa.

Ngoja nikuchekeshe kidogo na kisa cha wasaka fursa!

* kuna jamaa moja aliyemaliza chuo na kuamua kwenda katika mji fulani, aliwakuta watu wote wanatembea peku bila viatu, jamaa akaona hii ni fursa na kimya kimya akarudi mjini na kununua kontena la viatu ili akapige hela katika kijiji kile, alipofika akaandaa sehemu ili afanyie biashara yake ya viatu, cha ajabu hapakutokea mtu yeyote aliyeenda hata kuulizia bei ya viatu, kesho yake kuna wazee wakamfuata na kumwambia aitoe biashara yake kwa sababu katika kijiji kile ilikuwa ni jadi yao kutembea bila viatu*

Ukianzisha biashara kwa lengo la kutatua tatizo katika jamii uwe umefanya utatifi wa kutosha juu ya tatizo lile, Ukiwa na wazo la biashara ni busara kushirikisha wale watu unaowaamini vinginevyo yanaweza kukupata yale ya msaka fursa.

Biashara yenye lengo la kutatua changamoto katika jamii itakufanya ufike mbali sana, usianzishe biashara kwa lengo la kuonekana nawe pia ni mfanyabiashara bali jua kile unachoenda kukitatua katika jamii husika.

Wazungu walipoona tunachukia ngozi zetu nyeusi  walileta madawa ya kujichubua ili tuwe na ngozi nyeupe, hiyo ndiyo biashara. 

Walipoona watu wanachukia nywele za asili walileta mawigi, hii nayo biashara!

Fikiria biashara inayoweza kutatua tatizo katika jamii inayokuzunguka. 

Karibu tufikirie wote ndani ya jukwaa la fikra ukiwa na mimi Dady Lutelemla >+255620306815