Hakuna adhabu kali maishani kama kuishi ukiwa mkiwa wa kitu, mkiwa wa watu, mkiwa wa kazi na vitu vingine vingi. Hii ni adhabu kubwa sana ambayo kila moja huwa anaipitia katika maisha yake hasa akiwa na hali hizo nilizozitaja hapo juu.

Ni ukweli usiopindika kuwa watu husimama upand eww wako pale tu unapokuwa una kitu, unapokuwa na familia imara, unapokuwa na kazi nzuri n.k.

Unapokuwa na wazazi, pesa, na hata kazi utakuwa na marafiki na watu wengi sana wanaokuzunguka katika maisha yako, lakini usiombe yakukute upoteze vitu hivi utahangaika sana.

Kuna watu uliowadhania hawawezi kukutupa, watayeyuka na usijue walikopotelea, utasalitiwa na hata uliowaamini. 

Maisha kitu, maisha ni kuwa na kitu. Ukipata nafasi ya kuwa nacho jaribu kukitunza kwa ghalama yoyote ili kisipotee, Usijaribu kamwe kuichezea baraka uliyopewa na Mungu, kumbuka kuna mamilioni ya watu wanaitamani baraka hiyo kwa hiyo siku ikiondolewa majuto yanaweza kuwa rafiki yako.

Pasaka njema kwa watu wote!!

BONYEZA HAPA https://wa.me/255620306815 kuwasiliana nasi kupitia WhatsApp,  au BONYEZA HAPA dadylutelemla@gmail.com kuwasiliana nasi kupitia email  kwa ajili ya Maoni, Ushauri, Mapendekezo au Changamoto.