ISHI KAMA PENSELI ILI UWE MTU BORA.
Mtengenezaji wa penseli alipomaliza kuitengeneza penseli yake aliiambia mambo muhimu ya kuzingatia ili iweze kuwa penseli bora kabla hajaituma kuingia kazini kwa matumizi.
“Kuna vitu sita unatakiwa uvitambue, kabla sijakutuma kwenda kutumika, unatakiwa uviweke akilini vitu hivyo na usivisahau kamwe. Vitakusaidia siku zote na utakuwa penseli bora maisha yako yote.”
Alisema mtengeneza penseli.
MOJA----Utakuwa na uwezo wa kufanya vitu vingi, lakini kama utakubali na utaruhusu kuongozwa na mkono wa mtumiaji wako”
“MBILI" utapata maumivu makali kutokana na kuchongwa mara kwa mara. Lakini vumilia kwani itakusaidia kuwa penseli bora na kuandika vizuri.”
TATU--- utakuwa na uwezo wa kusahihisha makosa utakayo yafanya..
NNE---kitu pekee cha muhimu katika maisha yako ni kile kilicho ndani yako kwa sababu ndicho chenye uwezo wa kuandika. Hivyo kilinde
TANO---Alisisitiza mtengenezaji penseli, “kwenye kila sehemu utakayotumika, utaacha alama yako. Hata ikiwa ni kwenye sehemu ngumu au mbaya kiasi gani, ni lazima alama yako ibaki tuu.
“NA SITA-- Ipo siku utaisha na kupotea kabisa. Hivyo usiwe na hofu wala woga wala hudhuni uikaribiapo siku hiyo na ukaogopa kutimiza wajibu wako kwa kuhofia kuisha. Ukiogopa kuisha hautotumika na umuhimu wako hautonekana kwani hautatimiza wajibu niliokwambia kuufanya..
PENSELI ilielewa na kuahidi kuyakumbuka na ikaingia sokoni ikiwa na dhamira yake moyoni.
Sasa tutumie mfano huo wa penseli katika maisha yetu halisi. Ukivikumbuka vitu hivyo sita ilivyopewa penseli, utaweza kuwa mtu bora kabisa kwenye maisha yako yote.
Tumia mfano huu wa penseli upate ujasiri wa kutambua kuwa wewe ni mtu muhimu hapa duniani na umeumbwa kwa madhumuni maalumu na umepewa uwezo mkubwa sana na Muumbaji wako! Ni wewe pekee mwenye uwezo wa kutimiza kusudi ulilotumwa na Muumbaji WAKO.
Tzidi kulisogelea Jukwaa La Fikra tujenge nchi
Nicheki whasap kwa namba 0620306815
0 Comments