Washa taa ya ufahamu ndani ya ubongo wako na kisha jimulikie hadi ujione ulipo.
_______________________
Siku moja wakati wa sikukuu moja huko Yerusalem, Wayahudi walimzunguka Yesu na kumwambia, hebu tueleze ukweli hivi wewe ndo Yesu maana umezidi kutuzingua ujue! Hebu jitambulishe fasta!
Yesu akawachekiiiii, kisha akasema MIMI NA MUNGU TU KITU KIMOJA (Yohana 10: 30).
Wayahudi wakachukua mawe wamtwange. Yesu akashangaa, hawa jamaa vipi? Nimewafanyia mambo kibao. Sasa mnataka kunipiga kwa lipi hasa?
Wayahudi wakamwambia hatukupigi kwa mambo mazuri uliyotufanyia, tunakupiga kwa sababu ya kujilinganisha na Mungu. Hiyo ni kufuru!
Yesu akashangaaa,na kuwambia kwani siimeandikwa katika torati kwamba hata nyie ni miungu? (Zaburi 82: 6). _Tatizo lenu hamsomi_(hii nimechomeka)!
Ujumbe!
1. Tunaishi katika jamii ambayo watu watataka kukutambulisha watakavyo, watataka uwe vile wanavyopenda uwe, ukikataa watakupiga na kweli utapigwa, na wakupige tu! ( kwa sauti ya Mzee Pinda).
2. Usipojitambulisha vizuri watu watakutambulisha vibaya, watakuita mvivu, kibaka, malaya, muhuni, mlafi, tapeli, fala nk, ni nadra sana kutambulishwa vizuri. Hata rafiki yako atakuponda tu.
Wito
Anza kujitambulisha vizuri kwa kujitambua wewe ni nani. Jitafute hadi ujipate kisha piga kelele.
Washa taa ya ufahamu ndani ya ubongo wako na kisha jimulikie hadi ujipate.
Fanya hivyo kwa kuwa na Jukwaa La Fikra
Piga simu namba 0654836144 au whatsap namba 0620306815.
Karibu Jukwaani, wewe no mtu wa thamani sana.
0 Comments