Haijalishi Kucha Zinakatwa Mara Ngapi 

Bado Haziachi Kuota 

Ni hekima inayotuasa tusikate tamaa, dunia ni mapambano mpaka kufa. Mapambano ni ishara ya uhai. Hata kifaranga ili kitoke kwenye yai lazima kipambane mpaka lipasuke vinginevyo kitakufa. Vizuizi viko vingi lakini ni mwiko kukata tamaa. Katoto kadogo pamoja na kula myeleka ya kutosha kwa siku bado hakaachi simama dede. Kanajua kakiogopa mieleka hakata tembea kamwe! 

Hata kucha zinaporefuka hatukati vidole tunakata kucha. Tunatakiwa kuzifahamu changamoto na kuzitafutia majibu sahihi kwa sababu hakuna barabara isiyo na kona. 

Utamu wa mua fundo inasema methali ya kiafrika. Siku zote wayahudi hawaombi Mungu awaondolee changamoto bali wanaomba awape mabega makubwa ya kuweza kuhimili changamoto. 

Kurukaruka kwa maharage ndo kuiva kwake. Njia nzuri ya kumla tembo ni kwa kumkatakata vipandevipande. Huwezi kumla mzima. 

Acha hofu, songa mbele kwa sababu hofu haikusaidii chochote zaidi ya kukuondolea amani uliyonayo leo. “Mambo yako yanapokuendea vibaya, usiende nayo” alisema Elvis Presley. “Kabla ya kukata tamaa, jaribu tena” alisema Debasish Mridha. I am a slow walker but I don’t walk back. 

Hamasa Jukwaani na Dady Lutelemla. 

WhatsApp namba 0620306815.