*Wacha Niseme *
Leo ni siku ya wababa Duniani. Siyo siku maarufu sana kama siku ya Wanawake Duniani. Unajua kwa nini? Baba ni maarufu katika ubaya, mama ni maarufu katika wema. Tunakumbuka wema, hatukumbuki ubaya.
Lakini siyo kwamba baba hana wema na wala siyo kwamba mama hana ubaya. Hapana! Kila binadamu ana vyote; ubaya na wema isipokuwa, ubaya wa baba unajulikana sana kwa sababu mama anapenda kuusimulia na ubaya wa mama haujulikani kwa sababu baba anapenda kuuficha.
Yawezekana kabisa katika familia yenu kuna watoto siyo wa baba yenu lakini hautasikia baba yenu akiwasimulia hata siku moja. Na usidhani baba hajui. Anajua sana tu lakini amechagua kumsitiri mama.
Yawezekana kabisa na wewe hapo haupatani na baba yako kwa sababu mama alikusimulia ushenzi wa baba yako. Msamehe bure baba yako kwa sababu hakuna mkamilifu, sisi wote tuna mambo ya hovyo na wewe ukiwemo, sema tu Mungu katufichia!
Mfungue baba yako moyoni kisha mgonge hata kijizawadi cha kushitukiza popote alipo. Na kama aliishatangulia mbele ya haki, nenda katoe sadaka kanisani, msikitini, kwa wajane au watoto yatima kisha muombee Dady!
Mwanangu haya mambo utayapata katika app yako pendwa ya Jukwaa la Fikra pekee, fanya kusogeza na wengine pia.
Tuandikie kwa email dadylutelemla@gmail.com au WhatsApp namba +255620306815.
0 Comments