Mahusiano yako ni maisha, ukiyaharibu umekwisha. Hapa nazungumzia mahusiano ya aina tano; siyo mapenzi tu kama unavyofikiri.
*Moja: Mahusiano ya Kimapenzi*
Mapenzi yanakimbiza dunia, yakichacha dunia inakukimbiza. Linda sana mahusiano yako ya kimapenzi maana _*ukiwa na mpezi wa hovyo dunia utaionana nzito as if umepewa kazi ya kuibeba*._ Watu wakikuangalia wakajua unastress za mapenzi hawatakupa michongo. Wakupe michongo ukaiharibie kwenye mapenzi? Thubutu!
*Mbili: Mahusiano ya Kirafiki*
Umejenga mahusiano na marafiki wa namna gani? Marafiki wa stori za anasa au wa stori za utafutaji? Je uko na marafiki waliopigwa na maisha au walioyapiga maisha? Je uko na marafiki waliokuzidi akili au unaowazidi akili?
Watu wakijua uko na marafiki wa ajabu watakuona wa ajabu tu hivyo hawatakuwa na muda na wewe. *_Kumbuka ukiwa na marafiki wapuuzi watatu, jiandae kuwa mpuuzi wa nne!_* Achana na marafiki wa kuna mishe nasikilizia.
*Tatu: Mahusiano ya Mtaani Kwenu*
Mtaani watu wanakusemaje? Katibu mwenezi wa majungu? Unajulikana kwa ukorofi au uungwana? Unaitwa cha pombe wa mtaa au mama cha wote? Una faida mtaani au hasara tu?
Watu wenye interest na wewe wanapita mitaani kudadisi tabia zako kabla hawajafanya maamuzi. *_Unaweza kushinda interview lakini ukashangaa huitwi kazini._*
*Nne: Mahusiano na Ndugu*
Uko vipi na wazazi wako? Kaka zako je? Wajomba na mashangazi? Wanakuona nyau wa ukoo au msaada? Kuna mijitu ni mindugu ya kuzaliwa lakini haimbani chumvi. Mingine inarogana. _*Watu wakiishajua unatoka familia ya hovyo hakuna watakaopoteza muda na wewe!*_ Jirekebishe kwanza.
*Tano: Mahusiano Yako na Mungu*
Kanisani huendi, msikitini huendi, hata kwenye zile dini za Kiafrika huendi. Yaani upo upo tu. Unajiita nyutro! Jamii itakuona mbabaishaji tu. Chagua upande na uishi kwa sheria na taratibu za dini yako.
*Sita: Mahusiano na Jukwaa la Fikra*
Kwanza unajua kama nimetoa app mpya inayoitwa Jukwaa la Fikra? Jenga mahusiano mazuri na Jukwaa hili, utajenga mahusiano mazuri na Jukwaa hili kwa kutenga alau dakika 15 kwa siku ili ujijenge kiubongo pia.
Nitafute kwa namba ya WhatsApp +255620306815 tujenge mahusiano mema!
0 Comments