Kuna siri kubwa sana katika KUSUBIRI. 

Kuna mambo kwenye maisha huwa yanahitaji muda ili aidha UYAJUE au UFANIKIWE.

Kuna watu wamepoteza FURAHA yao kwa kufanya MAAMUZI ya papara.

Kuna watu WAMEISHI maisha yote wakijilaumu kwa kuchukua HATUA kwa sababu walikosa SUBIRA.

Unahitaji muda wa kusubiri ili KUZIJUA NIA halisi zilizoko ndani ya watu.

Kuna wengi watakuja karibu yako na watajionesha wema, usipowapa muda wa kutosha watakuumiza.

Kuna vitu unavitaka, ukikosa subira utatumia njia za mkato na utakiuka hata imani yako ili uvipate.....mwisho wa siku utavipata ila utabakia na majuto.

Ukiona moyo wako haujakuruhusu na unapata shida kuhusu mtu au kitu, jipe muda. 

Moyo wako una macho makali kuliko macho yako ya nje.

Uwe na Subira ili Usijute.