*Mke wa mtu siyo riziki ya msela kama wasemavyo vijana; mke wa mtu ni sumu!*

Dady Lutelemla

___________________________________

Kama unaipenda familia yako usitembee na mke wa mtu maana kuna wanaume wakijua hawatakwambia. Utashangaa tu wamekupiga tukio kama la Kigoma.

Jamaa wa Kigoma alivyogundua rafiki yake anakula mke wake hakumwambia kitu, waliendeleza urafiki akimlia timing ya kumuua. Akaja kuua familia nzima. 

Issue yenyewe ilikuwa hivi; jamaa baada ya kuthibitisha yaliyosemwa mitaani kwamba

kikulacho kinguoni mwako alianza michakato ya kumuua mlaji kimyakimya. 

Siku ya mauaji walishinda wote. Walizunguka mitaa mbalimbali ya kijiji cha Kiganza wakila na kunywa akimlia timing ya kumuua.

Ilipofika usiku kabla lengo lake la kumuua halijatimia alimuomba alale kwake kwa hoja kwamba usiku umeingia na hataweza kurudi nyumbani. Akakubaliwa kulala kwa sababu urafiki ni kufa na kuzikana.

Usiku wa manane akaamka na kuwacharaza mapanga familia nzima. Alitumia panga lililokuwa ndani. Walikuwa watu saba! Wote wamezikwa, muuaji yuko jela. Waungwana tukapata la kujifunza. Mke wa mtu sumu.

Vijana wanakwambia kabla ya kushikwa mke wa mtu haiwezi kuwa sumu. Hilo ni zari tamu msela. Ukishikwa ndiyo hugeuka kuwa sumu ya msela. 

Kuna mwanaume akigundua unamuibia anakupa tahadhari uache. Wengine hawanaga tahadhari. Akigundua anamaliza labda awe hampendi mke wake.

Ukiona unachepuka na mke wa mtu na hujafanywa kitu kuna matatu. Ama jamaa hajajua au amejua anakulia timing au hampendi mke wake!

Kuna watu waliishawatoa moyoni wake zao kiasi kwamba hata wakilala nje poa tu. Kuna mwanaume analala kitanda kimoja na mke mpaka asubuhi bila hata kumtomasa.  

Lakini hata kama hamtomasi, bado huna haki ya kunywea maji kwenye kisima cha watu. Awe anampenda au hampendi. We jua mke wa mtu ni sumu tu. Kwahiyo

Usitumie cheo chako kama fimbo ya kuchapia wake za watu! Siku yakikufika cheo hakitakusaidia. Utajuta kwa nini ulikubali hicho cheo.

Usitumie uhandsome wako kama fimbo ya kuchapia wake za watu wanaopagawaga na mahandsome. Siku ya kikufika utajuta kuzaliwa handsome.

Usitumie urafiki wako kama fimbo ya kuchapia wake za rafiki zako waliokosa adabu. Siku yakikifika urafiki ndiyo utarahisisha kifo chako.

Usitumie umaskini wa mwanaume mwenzako kumchapia mke wake. Siku akigundua utaelewa hakuna maskini dhaifu mbele ya mke wake.

Usitumie uchawi kama fimbo ya kuwachapia wake za watu. Siku yakikufika utalewa kwa nini mchawi haagizi tembele! Anaagiza kuku mweupe.

Usitumie nyota ya kupendwa kama fimbo ya kuwachapia wake za watu. Siku yakikufika utaelewa si kila nyota ni njema! Nyota nyingine ni majaribu.

Usitumie ubusy wa kazi wa mwanaume mwenzako kama fimbo ya kumchapia mke wake. Akigundua atakuwa busy na wewe mpaka akufinyange upya. Shauri lako. 

Usitumie ugonjwa wa mwanaume mwenzako kama fimbo ya kumchapia mke wake wake! Akigundua atakutia ugonjwa wa kudumu. Kumbuka mtaani kuna wahuni ukiwapa laki moja tu wanakutia kilema cha kudumu.

Usitumie uzuri wa mke wa jamaa yako kama fimbo ya kumchapia mke wake. Hii ni mbaya. Kisa tu umesikia kuoa mke mzuri ni sawa na kulima miwa karibu na shule ya msingi. Kama unadhani mke wa mtu ni muwa kakate utafune uone kama utameza!

Usitumie udhaifu wa nguvu za kiume za mwanaume mwenzako kama fimbo ya kumchapia mke wake. Yakikukuta utajilaumu kwa nini una nguvu nyingi za kiume.

Usitumie gari lako kama fimbo ya kuwachapia wake za watu wanaoshobokea vijiliftlift. Siku ukikamatwa utajuta kwa nini ulinunua hilo gari.

Usitumie umbo lako la gym kama fimbo ya kuwachapia wake za watu wanaopagawa na vifua vipana. Siku ukikamatwa utajuta kwa nini uliwekeza kwenye gym.

Usitumie kitengo chako  cha usaili kama fimbo ya kuwachapia wake za watu wanaokuja kuomba kazi kwa kuwapa maswali magumu ili wakuhonge rushwa ya ngono. Yakikukuta utajilaumu kupewa kitengo hicho!

Usitumie kitengo chako cha kutoa mikopo ya wajasiriamali kwa wanawake kama fimbo ya kuchapia wake za watu wanaotaka mikopo. Siku likibumburuka utajilaumu kwa nini ulikubali hicho kitengo.

Usitumie bodaboda yako kama fimbo ya kuwachapia wake za watu wanaopenda kamseleleko. Ukikamatwa unaweza usiendeshe boda boda maisha yako yote.

Usitumie ufundi wako wa kutongoza kama bahati ya kutembea na wake za watu. Kwanza utongoza wake za watu na kukubaliwa siyo bahati. Ni balaa. Muombe Mungu akuepushe! Majuto ni mjukuu!

Acha tabia za kuwa na relationship na wake za watu maana safari moja uanzisha nyingine. Kutembea na wake za watu kuna laana pia. Madili yako hayawezi kukaa kwenye mstari kama unashea penzi na wanaume wenzako! Huko mikosi ni mingi.