*Chagua Huzuni Uwahishe Kifo Chako; Chagua Furaha Ucheleweshe Kifo Chako!*
Dady Lutelemla
________________________
Kuna vitu ukiacha kuviwaza na vyenyewe vinaacha kukusumbua!
Kuna mambo ukiacha kuyafuatilia na yenyewe yanaacha kukuumiza!
Kuna vyeo ukiacha kuvifikiria na vyenyewe vinaacha kukuumiza!
Kuna watu ukiacha kuwafikiria na wenyewe wataacha kukuumiza!
Kuna magonjwa ukiacha kuyafikiria na yenyewe yanaacha kukuumiza!
Kuna watu wana magonjwa kibao, lakini hayawaumizi kwa sababu hawajui kama wanayo.
Kuna mtu ameishi na gonjwa fulani kwa miaka kibao lakini alikufa siku alipogundua analo!
Kinachoua siyo ugonjwa, ni mawazo kuhusu ugonjwa!
Kinachoua siyo shida, ni mawazo kuhusu shida,
Kinachoua siyo mapenzi, ni mawazo kuhusu mapenzi,
Kinachoua siyo huzuni, ni mawazo kuhusu huzuni!
Kinachoua siyo madeni, ni mawazo kuhusu madeni!
Tafuta furaha kwa namna yoyote,furaha ni hisia na uamuzi!
Usisubiri hadi upate hela ndiyo ufurahi, furahi tu!
Usisubiri hadi upate kazi ndiyo ufurahi, furahi tu,
Usisubiri hadi akukubalie ndiyo ufurahi, furahi tu hata bila kukubaliwa,
Usisubiri kupata cheo ndiyo ufurahi, furahi tu maana unaweza kufa hujapata cheo!
Usisubiri hadi uolewe ndiyo ufurahi, furahi tu hata ukiwa single, furahi tu hata kama umri umekwenda na mume hujapata!
Maisha ni kuchagua, ukichagua kufuatilia huzuni jiandae kufa vibaya, ukichagua kufuatilia furaha lazima uishi kwa furaha.
Jenga utamaduni wa kufurahi hata kwenye hamna, furaha ni tiba ya vingi!
Karibu Jukwaani mpendwa.
0 Comments