Tujifunze kutenda miujiza kama Bwana Yesu! Kutenda miujiza siyo mpaka kumuombea kiwete atembee na kiziwi asikie. 

Hapana hata kumlipia mtu gharama za matibabu akapona ni muujiza kwake. Hata kumlipia mtoto ada akarudi shuleni ni muujiza kwake. Hata kutatua dharula ya mtu na kumuokoa na aibu iliyokuwa mbele yake ni muujiza. 

Unajua katika jamii zetu ukishindwa kuhudhuria msiba wa ndugu yako kwa kukosa nauli utaonekana wa hovyo wakidhani umepuuzia. Kumbe kamanda huna hata jero na ukizingatia watu wengi hatuna utamaduni wa kutunza akiba.

Halafu hakuna atakayekuuliza kwa nini hukufika msibani dadeki. Wanachojua wewe ni Mtumishi wa Umma, unadharau misiba. Halafu msiba umetokea kijijini!  


Siku Moja Bwana Denis Mpagaze alimtembelea jamaa yake Mjeshi Pasiansi Mwanza wakati huo anaishi Nyegezi. Kufika nyumbani kwa jamaa yake akakuta kikao cha familia, wanajadili namna ya kupata nauli ya kumfikisha mtoto wa kaka wa huyo jamaa yake kwenye msiba wa baba yake. Yaani jamaa yake alikuwa anaishi na mtoto wa kaka yake. 

Halafu nauli yenyewe ni Sh 12,000 tu mtu mmoja, miaka ya 2000. Basi akawapatia Sh 30,000 ili waende msibani yeye na mtoto. Alivyokabidhi ile pesa, jamaa yake alisimama, akamkumbatia kwa nguvu, kisha akasema “Denis! We ni mshenzi!” Mungu akubariki sana.” Asubuhi wakaenda msibani Kibondo. Hapo Denis alitenda muujiza.  


Nenda na wewe katende miujiza. Jamii haitakukumbuka kwa utajiri ulionao, jamii haitakukumbuka kwa uzuri ulionao, jamii haitakukumbuka kwa umaarufu ulionao; jamii itakukumbuka kwa miujiza uliyowatendea watu. Jamii itakukumbuka kwa jinsi ulivyogusa nyoyo za watu. Yesu anakumbukwa mpaka leo kwa sababu aligusa nyoyo za watu. 

Yesu alitenda miujiza kibao. Yesu alimfufua Lazaro, dada zake wakalia kwa machozi ya furaha. Wewe huna nguvu ya kufufua mtu lakini ukimlipia gharama za matibabu mgonjwa mmoja akapona hapo utakuwa umemfufua kiana. Believe mimi! Mungu hatakusahau.

Tenda miujiza kwa kushare Jukwaa La Fikra lifike mbali, kwani kwa kufanya hivyo nitakushukura sana na Mungu hatakusahau. 

Nitafute kwa WhatsApp namba +255620306815 au piga kwa namba +255654836144 ili tujadili namna ya kuyenda miujiza katika jamii.