*Maisha ya hisia yanawatesa watu wengi kuliko maisha ya uhalisia.*

            Dady Lutelemla 

_________________________

Mwenzako akiondoka akachelewa kurudi unahisi kachepuka,moyo unakuuma kweli! Kumbe yawezekana kala nauli akitegemea kusongesha, ikagoma. Shukuru kuna msamalia kamsaidia.

Unampigia simu hapokei unahisi anacheat  unaumia kweli! Kumbe maskini ya Mungu wakati unampigia simu ilikuwa kwenye silent, amekuja kuiona hana salio hata la *kudipu*🤭🤭! 

Unamsalimia haitiki, unahisi amekudharau unaumia kweli! Kumbe ni kiziwi.

Unamuomba pesa anakwambia hana unahisi amekunyima unaumia kweli! Kumbe ni kweli hana hata jero.

Unamuona mwenzako yuko online mpaka saa nane za usiku lakini hachati na wewe unahisi kakudisi, unaumia kweli. Kumbe mwenzako kasinzia muda, ni vile tu alisahau kuzima data!

Unamtumia nauli, halafu haji unahisi amekataa unateseka kweli. Yawezekana hakuja kwa sababu nauli ile amenunua chakula nyumbani maana walishinda njaa!

*Achana na hisia upunguze mateso*

Nicheki kwa WhatsApp namba +255620306815 au piga simu namba +255654836144 tuchonge mengi.