Mabinti zetu wanashindana kubeba mimba pasipo kujiuliza watoto wao wataishije katika dunia hii iliyojaa raha na karaha. 

“Nasubiri tu kakiacha kunyonya nakapeleka kwa bibi yake kijijini” ni maneno ya vibinti vilivyoamua kuwekeza katika kuzaa na kutelekeza watoto kwa wazazi wao. Kwa sababu ya haraka watoto wanakuja duniani kusota. Hii ndio “Born to Suffer” aliyoimba Lucky Dube. 

Watu makini wanauliza maswali kabla ya kutafuta majawabu wakati wengine wanatafuta majawabu kwanza halafu maswali baadaye. Ni ajabu sana. Uvivu wa kuhoji umefanya vyama vya siasa hapa Tanzania kuwa vya matukio tu. Havina ajenda! Shida wanasiasa wamekuwa wataalamu wa kutoa majawabu bila kujua maswali yaliyoulizwa. Kitendo cha mbunge kutoa ahadi kwa wananchi wake kwamba atajenga shule, ataleta umeme na huduma nyingine za kimaendeleo kwa pesa ya kuomba serikalini ni sawa na kufanya mtihani usio na maswali. 

Wengi tumeshindwa kujikwamua maishani kwa sababu tunaanza na gia ya kushindwa. Tumebeba majawabu kwenda kujibu mitihani isiyo na maswali. Utatoaje majibu kabla hujajua swali? Profesa Edwini R Keedy wa chuo kikuu cha Pennyslavia alizoea kuanza somo lake la kwanza kwa darasa jipya kwa kuandika namba mbili ubaoni yaani 4 na 2. Baada ya kuandika namba hizo mbili aliuliza; “Jibu ni ngapi?’ Mwanafunzi mmoja alisema ni sita, mwingine akasema ni mbili na mwingine alisema nane. Baada ya majawabu yote hayo profesa akasema,“Nyote mmeshindwa.” Bila kujua swali huwezi kujua jawabu. Na hicho ndicho tukifanyacho watanzania tulio wengi. 

Dhambi kubwa duniani kuliko zote ni kutoa majawabu ya swali kabla ya kujua swali limeulizwaje.

Jukwaa la fikra ni sehemu pekee ya kujifunza na kujua haya yote.

Nitafute kwa WhatsApp namba +255620306815 au nipigie simu tuyajenge.