Ngoja Niwakeree!
Hoja za maskini zinatisha, halafu zinatia huruma. Maskini wa akili akiongea jambo utabaki kujiuliza hivi na huyu kamkosea nini Mungu? Mbona hana wivu wa kimaendeleo na wakati anayataka? Unadhani tatizo ni nini? Tatizo nikwamba! Sehemu kubwa ya ubongo wake imejaa fikra za "Sizitaki mbichi hizi" huku udenda ukimtoka. Hizi ni akili za Sungura.
Paza sauti kuzikemea kwa nguvu zako zote, akili zako zote na moyo wako wote, maana unakera!
Utaskia, "Pesa nyingi za nini na wakati wote tunakwenda chooni? Toba! Eti Hata uwe na magari mengi ya kutembelea, chooni utakwenda kwa miguu". Mtumee! Sina pesa lakini nalala usingizi. Yerewii! Hivi unapataje usingizi kodi ya nyumba imeisha wiki iliyopita? Unaweza sema shetani aliishamnyofoa ubongo huyu jamaa kumbe upo sema umenoki. Kwa mawazo ya namna hii unatokaje kwenye umaskini? Yakatae kwa vitendo na matendo, yakatae kwa sala na maombi. Maana kama ni kuomba, unaomba hadi mbingu zinatakisika kwa kelele zako zisizokuwa na hoja!
Kumbuka imeandikwa,leteni hoja zenye nguvu na siyo kelele za nguvu. Wewe unabweka!
Nauchukia umaskini kwa sababu unakula ubongo! Mtu mwenye fikra za kimaskini amebarikiwa maneno mengi ya kumpatia ahueni kwenye hamna. Utasikia, "Simu ni simu tu ilimradinawasiliana." Nyumba nzuri kitu gani? Kwani usingizi si ule ule?
Unataka uniambie usingizi wa aliyelala kwenye nyumba yenye choo cha shimo ndani na aliyelala kwenye nyumba yenye choo cha maji ni sawa? Labda chizi. Maana kwa chizi jana na leo havitofautiani.
Ukiwa na fikra za namna hii zitakufanya ufubae kwa umaskini. Utaitwa bingwa wa shida. Hakuna bingwa wa shida hebu nenda katafute pesa!
Hata lugha za mwanaume mashine huwezi kuzikuta kwa serious guys.Utazikuta kwenye vijiwe vya vijana maskini. Hawana kazi ya kufanya zaidi ya kushindanisha wanawake wenye makalio makubwa wanaopita barabarani.
Maskini bwana. Utaskia Mungu amenibariki watoto saba, lakini anashindwa kuwahudumia. Anasema kila mtoto anakuja na riziki yake. Hivi kweli ni Mungu gani huyu akupe baraka usiyoweza kuitunza? Watoto wanakula msoto hadi wanamuuliza mama, baba atakufa lini? Maskini bwana. Hawa ndo hutuzalia akina born to suffer!
Ukimtembelea maskini na gari kali ataishia kusema aliyekupa wewe ndo kaninyima mimi. Badala na yeye kumuomba huyo aliyemnyima ampe gazi zuri anaishia kujenga hoja dhaifu ili kujustify njaa zake. Kauli kama hizi hukujengea matumaini ya kuendelea kuwa maskini. Huwezi kushindana kama una kirusi cha namna hii kichwani. Unahitaji kuformat kichwa!
Nimepanda jukwaani kwa kuwakera, samahani sana ila nicheki kwa whasap namba +255620306815 au nipigie kwa namba +255654836144.
0 Comments