Ni ukweli usiopingika kwamba ili utoke chini na kufikia mafanikio yako makubwa lazima kuna changamoto uzivuke.  Mafanikio yanapimwa na uwezo wako wa kutatua changamoto. Kadri unavyotatua changamoto unazopitia ndivyo unavyozidi kupiga hatua kuelekea mafanikio makubwa.Leo nataka kukushirikisha njia mbili muhimu zitakazokusaidia kutatua changamoto yoyote unayopitia.

Njia ya kwanza: Ushauri kutoka kwa watu unaowaamini

Ukweli ni kwamba changamoto yoyote unayopitia kuna watu waliokutangulia walishaipitia. Hakuna changamoto ya mafanikio ambayo ni mpya.

Kwa hiyo badala ya kukaa pekeyako ukiangaika kutatua changamoto unahitaji kuwatafuta watu unaowaamini. Watu ambao wamefanikiwa kwa kupitia changamoto kama zako.

Wengine wanawaita mentors au kocha. Kumbuka hapa sio kila mtu anatakiwa kukushauri. Ushauri wa wengine utakupoteza. Tafuta watu ambao unawaamini.

Watu ambao wanakupa hamasa ya wewe kwenda mbele. Watu ambao wameshapiga hatua kubwa kwenye safari yao ya mafanikio. Utashangaa kwa ushauri mzuri wa bure watakaokupa.

Njia ya pili: Kusoma vitabu

Kuna maarifa mengi yamefichwa kwenye vitabu. Kama usomi vitabu kuna vitu vingi sana unakosa. Moja ya kitu ambacho utakipata kwenye vitabu ni mbinu za kutatua changamoto.

Kama nilivyosema hakuna changamoto mpya duniani. Changamoto nyingi unazopitia, mbinu za kuzitatua ziko kwenye vitabu.Kama umekuwa hauna tabia ya kusoma vitabu, anza kusoma vitabu leo, angalau hata kitabu kimoja kwa mwezi.

Watu wengi wanasema watanzania wengi ni wavivu wa kusoma vitabu. Wewe jitoe kwenye hilo kundi la wengi. Jitofautishe kwa kusoma vitabu na utapata mbinu nyingi za kutatua changamoto unazopitia.

Hizo ndio njia mbili muhimu zinazoweza kukusaidia kutatua changamoto yoyote unayopitia. Kumbuka changamoto nyingi unazopitia kuna waliokutangulia walishazipitia.

Badala ya kuangaika kutatua changamoto pekeyako,tafuta ushauri kutoka kwa watu unaowaamini na soma vitabu kupata mbinu za kutatua changamoto unazopitia.

Hamasa Jukwaani na Dady Lutelemla!

Whatsap namba +255620306815