Mwanangu kuna vitu hapa duniani ambavyo hutafutwa kwa nguvu, bidii na maarifa yote lakini kamwe usiitafute heshima kwa namna hiyo! 

Mwanangu kamwe heshima haitafutwi ila hujengwa na wewe mwenyewe, ukitaka upate heshima katika mazingira ya kazi ni lazima ujiheshimu wewe mwenyewe. Ukitaka watu wakuheshi katika nyanja yako ni busara kubwa ukajenga heshima yako juu ya kile unachokifanya! 

Heshima huja bila kuitwa, mwanagu usihangaike kuwaita watu hawana heshima huku ukiwa wewe mwenyewe hauwaheshimu, 

Mwanangu toka nimekuasa kubadilisha pHd kuwa mkate ukekuwa unaitaka heshima kwa nguvu zote, unatukana watu ofisini kisa tu hawajakusalimia huku wewe unawapita kama gari lisilo na breki. Unaniaibisha sana mwanangu, unafedhehesha na hiyo siyo namna nzuri ya kutafuta mkate!

Salimia watu mwanangu, jishushe chini kwa kila jambo, waheshimu watu wa kila rika, wape thamani, kisha uone kama kuna heshima haitakufauata!

Tengeneza mifereji ya kupata heshima mwanangu!

Mwambie na mdogo wako kuwa ujumbe huu nimeuacha Jukwaani> +255620306815.