USIKIMBIE KUPANDA KWA MACHOZI 
Zab 126:5 inasema "Wapandao Kwa machozi watavuna kwa kelele za Furaha."
Ni kweli unataka kufika Mbali...Ni kweli unataka kufanikiwa, Ni kweli unataka kuwa mfano wa kuigwa
SASA INAKUWAJE UNAKUBALI MAJIBU MEPESI KWA MASWALI MAGUMU? 
Majibu mepesi
- yanazuia uwezo wa kufikiri zaidi
- yanazuia upeo wa kuona zaidi
- yanazuia Uthubutu 
- yanazuia Ubunifu
- yanakufanya urelax 

- yanazuia commitment
- yanazuia uwajibikaji
@Kumbuka cheap is very expensive.... Vitu rahisi rahisi vinagharimu sana mbele ya safari.


@Zingatia hili kuwa Misingi ya jambo hutoa taswila ya Muelekeo au Hatma ya jambo husika
-Kupanda Kwa machozi maana yake ni kuweka misingi imara juu ya maono uliyo nayo hata kama inakugharimu / hata kama inakuumiza
- kupanda Kwa machozi ni kufanya vitu Kwa uhakika na sio Kwa kukurupuka 
- kutokufanya jambo Kwa kuwa umeona mwingine kafanya

USIPENDE NJIA ZA MKATO
@ Kumbuka njia za mkato( shortcut ) ni temporary yaani sio njia za kudumu sasa unakuwaje na MAONO alafu unategemea njia za mkato ambazo sio za kudumu.

@ It may take you sometimes to build your strength ( foundation) yaani inaweza kukugharimu muda mrefu kuweka misingi imara ya jambo na wengine wakaona unachelewa Kwa kuwa wao labda walipita njia za mkato wasijue sio njia za kudumu, siku wanayokuja kushtuka umeinuka na unakwenda Mbali Kwa speed.

Njia za mkato nazifananisha na DARAJA LA BARAFU.... U know what! Jua likiwaka hakuna kuvuka maana Daraja linageuka kuwa mto, na Biashara inakuwa imeishia apo.
Zingatia - kutokuyakatia tamaa maono yako
- usiyumbishwe na vitu ambavyo sio halisi 
- usiyumbishwe na vitu vya muda mfupi
- usivunjwe moyo na vitu vinavyotokea na kupotea
MAONO YAKO YANAWEZA KUCHELEWA SANA YANGOJEE... Habakuki 2:3 anasema "Maana njozi hii Bado ni Kwa wakati ulioamriwa, "ijapokawia, ingojee, Kwa kuwa haina Budi kuja, haitakawia."
Njozi yako itatimia, hakikisha tu unaweka misingi imara.

Karibu katika Jukwaa la fikra tujenge nchi!
 Wako Dady Lutelemla >+255620306815