Wajibu wa daktari ni kutibu; uponyaji anatoa Mungu;

Wajibu wa mwalimu ni kufundisha; uelewa anatoa Mungu;

Wajibu wa Mchungaji ni kuhubiri; wokovu anatoa Mungu;

Wajibu wa kulala ni wako; usingizi anatoa Mungu;

Wajibu wetu ni bidii kazini; mafanikio anatoa Mungu;

Wajibu wa dereva ni kuendesha; kufika ni majaaliwa ya Mungu;

Wajibu wetu ni kuoana; kupata watoto ni wa Mungu;

Wajibu wetu ni kuomba; majibu ni kazi yake Mungu;

Kabla ya kuomba lazima ujitathmini kwanza kama umetimiza wajibu wako. 

Kumuomba Mungu akuponye na wakati hujafika kwa daktari ni utani; 

Kumuomba Mungu akupe utajiri na wakati unalala muda wote ni utani;

Kuomba ufaulu mtihani na wakati husomi ni utani;

Kuomba amani ya ndoa na wakati huna adabu kwa mpenzi wako ni utani; 

Siyo kwamba Mungu hawezi kufanya bila wewe kufanya. Hapana! 

Mungu ni Shirikishi. Anaheshimu uwezo aliokuwekea ndani yako;

Wewe fanya kulingana na urefu wa kamba yako, kisha mtwike yeye;

Mungu alipoumba mto, alituachia kazi ya kujenga daraja

Angeweza sema alitupa heshima ya kushiriki.

Hamasa Jukwaani, nicheki kupitia https://wa.me/message/53VBBZFVGUZWF1