Kuwa na biashara bila kuitangaza ni sawa na kumkonyeza msichana gizani!


Denis Mpagaze

_______________________________


Waanzishao biashara ni wengi lakini wazitangazao ni wachache ndiyo maana hazikui na nyingine zinakufa kibudu. Matangazo ni moyo wa biashara; ukisimama biashara inasimama; ukizunguka biashara inazunguka. Matangazo ni sumaku ya kuvuta watu waikubali huduma yako. Katika biashara watu hao wanaitwa wateja; katika michezo washabiki; katika siasa wapiga kura; katika dini waumini; katika elimu wanafunzi; katika ajira wafanyakazi.


Kumshawishi mtu atoe pesa kununua kitu ambacho hata asipokinunua hafi inahitaji akili kubwa ndiyo maana mwaka 1925 Bruce Fairchild Barton, Bingwa wa Matangazo kutoka Marekani akamtangaza Yesu kuwa The Marketing Genius wa wakati wote kupitia kitabu chake cha The Man Nobody Knows. Yesu aliondoka kitambo sana lakini kila kona ya dunia kuna watu wanakula na kunywa vizuri tu kupitia Jina la Yesu wao. Mpaka sasa unaambiwa hakuna movie umeyouza sana duniani kama movie ya Yesu.  


Mwenzangu umeanzisha huduma ikafa hata kabla hujafa pamoja na uwekezaji mkubwa ulioufanya. Ulifungua grocery kwa mbwembwe, tiles za vioo na Wifi hadi chooni lakini umefunga. Unajua ulikosea wapi? Hukutangaza. Uliamini kizuri chajiuza; kibaya chajitembeza, ukatulia na kizuri chako kijiuze; matokeo yake yakakushangaza; kizuri kikadola huku wenye vibaya wakipiga hela.


Sikiliza mpendwa. Zama zimebadilika. Siku hizi vizuri na vibaya vyote vinajitembeza. Kujitembeza ndiyo kujitangaza kwenyewe.


Pengine umesoma vizuri; unajua vingi lakini unakufa njaa kwa sababu hawakujui. Kuna dogo nilikutana naye Songea, baada ya kupiga naye story niligundua ni bingwa wa magonjwa ya kike hasa kansa ya shingo ya uzazi, nikampeleka ofisini kwangu,pale Redio Jogoo, nikamkabidhi kwa mtangazaji nguli, wakaanda kipindi cha afya ya shingo ya uzazi, dogo akatoa somo, siku hiyo alipokea simu na meseji kidogo afe; dogo akawa maarufu ghafla, hivi tunaongea amehamishiwa Muhimbili na juzi nimemuona akitoa lecture kuhusu kansa ya shingo ya uzazi pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Matangazo!


Faida za kujitangaza ni nyingi kuliko hasara. Kufanya biashara bila kuitangaza ni sawa na kumkonyeza msichana gizani! Huwezi kumpata. Unatakiwa kutangaza biashara yako muda wote. Bila kutangaza huuzi. Biashara ni mchezo wa namba; jinsi idadi ya watu wanaojua biashara yako kuongezeka ndivyo chansi ya kuuza inavyozidi kuongezeka.


Jinsi unavyojitangaza ndivyo anavyojihakikishia soko la uhakika. Tangaza mara kwa mara. Matangazo ni moyo wa biashara, yakisimama biashara inakufa. Cocacola imedumu miaka kibao kwa sababu ya kujitangaza. Tigo, Airtel na voda wanatikisa kwa sababu wanajitangaza; TTCL imesinzia kwa sababu hawajitangazi kivilee. Labda kwa kuwa ni mali ya umma; wauze wasiuze wafanyakazi watapata mishahara.  


Kutangaza biashara ni kuipa umaarufu biashara yako ipate soko, vinginevyo utaifunga na mikopo ya watu ushindwe kulipa. Biashara si uchawi. Biashara ni pata potea. Usipopoteza huokoti. Usipopoteza hela kwenye matangazo hautaokota hela kwenye mauzo. Hata uwe na duka limejaa bidhaa mpaka nyingine unazikanyaga kama hauna wanunuzi hilo siyo duka; hiyo ni stoo ya bidhaa.


Ukiishaingia kwenye biashara huwezi kukwepa matangazo. Tangaza acha utani aisee. Kwanza unatakiwa kuelewa unapofungua biashara umetangaza vita na wateja. Wateja siku zote wanataka vitu vya bei ya chini, kamserereko, tena ikiwezekana wanataka uwape bure kabisa utadhani mtaji ulioutoa mbinguni; ndiyo maana ukimzidishia chenji mteja wako hakuonei huruma. Anakupiga.


Matangazo ndiyo silaha yako, maana yatakuletea wateja wengi, mzunguko utakuwa mkubwa hata ukiuza kwa bei ya chini bado utapata faida na biashara haitakufa. Wenye akili wanafanya hivyo. Wanatengeneza faida ndogo katika mzunguko mkubwa kwa sababu small is beautiful.  Kikubwa tangaza, tangaza, tangaza.


Siku hizi ni rahisi sana kutangaza. Kama huwezi gharama za televisheni, redio na magazeti basi tumia hata bodaboda. Hawa boda boda usiwachukulie poa. Ukiwatumia unatoboa. Hawa ndio wanaoulizwa na wageni na wapita njia huduma fulani iko wapi. Watu wa guest houses wanawatumia sana. Hata ukitaka kujua unashare na nani waulize hawa jamaa. Wanajua mengi, ila huwa hawasemi hadi uwaulize. Na tena usiwaulize kizembe.  Sijui naeleweka?


Ongea nao vizuri. Wapige hata ofa za mafuta siku moja moja. Lita moja ya mafuta atakuletea hadi wale wateja wa majumbani wanaomtuma, nyanya, vitunguu, gesi na pampasi. Utasikia mtu anainua simu yake na kutoa maelekezo kwa bodaboda wake, “niletee mshumaa; niletee nyama; niletee mboga”.  Tumeendelea, kila mtu anadereva wake. Bodaboda.


Sasa imagine umeunda urafiki na bodaboda wa kutosha unadhani wakitumwa watakwenda wapi? Kaa vizuri na boda. Boda hawana gharama. Wape hata vocha za jerojero uone. Hiyo ndiyo biashara ya tumia pesa upate pesa.Wakati mwingine hatupati wateja si kwa sababu wateja hawapo ila ni kwa sababu wateja hawajui tupo.


Paketi moja la pipi lina pipi nyingi mnooo. Tenga moja dukani kwako; watoto wakitumwa dukani unampa moja, amini nakuambia watawaambia na watoto wenzao hata wakitumwa duka lingine hawataenda. Watakuja kwako.  Watoto nao dili la biashara yako kama boda tu. Hawa wanatumwa sana na wazazi wao, jamaa zao hata walimu wao. Yote haya ni matangazo.


Yesu alikamata wanaume 12, akakaa nao vizuri, wakaitangaza huduma yake, leo zaidi ya watu bilioni mbili na nusu duniani ni wafuasi wa Yesu. Yesu hakufika sehemu zote za dunia lakini huduma yake ilifika. Biashara ni matangazo.


Siyo pipi tu kwa watoto. Toa hata ofa ya hereni feki kwa wateja wa kike wanaokuja kununua kwako. Kwani seti ya hereni shilingi ngapi bana? Toa pesa upate pesa. Fanya hivi. Nunua spika ya mchina, rekodi sauti murua ya kiume, ifungulie siku nzima; “ Mwanamke hereni, leo bosi kachanganyikiwa; anamvalisha kila mteja hereni….kama huna hereni ingia ndani jichagulie hereni uipendayo, kisha nunua kitu chochote dukani, upate hereni pea moja bureeee; karibu, karibu, karibu,usipite bila kuingia ndani hata ushangae tu kidogo”…


Kisha inaingia sauti tamu ya kike ...kina kaka karibuni muwachagulie mabebeeeez wenu hereni za bureee kabisa…nunua kitu chochote upate pea moja bureeeee…mpelekee mrembo!!!!


Matangazo nayo yanaufundi wake. Siyo huduma ya kike unaitangaza kwa sauti ya kike, utapishana na fursa. Sauti ya kike inaleta ladha tamu kwa huduma za kiume; sauti ya kiume inaleta ladha tamu kwenye huduma za kike! Chukua hiyo! Wateja watatu wanne wakiingia kwako na kutoka wamevaa hereni wakaingia mtaani hesabu ushindi. Usiangalie hela unayopoteza leo katika matangazo; angalia hela utakayoipata kesho kutokana na matangazo.


Kufungua biashara bila kuitangaza ni sawa na kuwasha taa na kuiweka chini ya kitanda. Huko itawamulikia mende wazaane vizuri wakale nguo zako. Halafu mende wasivyokuwa na adabu, wanasubiri uko na watu wa heshima ndio anatoka kwenye mfuko wa shati na kuingia kwenye mfuko mwingine.


Biashara ni matangazo. Unaweza kuwa na bidhaa nzuri usiuze kwa sababu hujaitangaza lakini mwenye bidhaa ya hovyo akauza hadi akachoka kwa sababu tu ameitangaza. Kwani mara ngapi umeangukia biadhaa ya hovyo, tena kwa bei ya juu na wakati bidhaa kama hiyohiyo inauzwa cheap mtaa wa tatu?  


Unajiita dalali halafu unalia njaa. Hauko serious. Madalali wenzako kila siku wanaokota hela tu. Kajitangaze. Usiassume kwamba watu wanakujua. Kuacha kutangaza ili kusevu pesa ni sawa na kusimamisha saa yako ili uokoe muda alisema Henry Ford. Siku hizi watu wanataka kwanza kujua kabla ya kununua. Enzi za kununua kwa kukurupuka zimeisha. Pesa imekuwa ngumu.


Jieleze mbele ya mteja akuelewe. Tumia lugha rahisi na yenye ushawishi. Mteja ni mfalme. Mfalme hanuniwi. Mfalme anabembelezwa. Jishushe mbele ya mteja wako. Yesu alijishusha. Ndiyo. Aliwaosha hadi miguu wanafunzi wake! Yesu hakuwa boss. Katika hili wafanyabiashara wengi wanafeli sana. Hawana lugha ya mteja ni mfalme. Wengi wana lugha za kijeshi.


Sikiliza, kama huwezi kutabasamu usifungue duka. Kuna duka niliacha kwenda kununua vifaa vya ujenzi kwa sababu siku zote muuzaji amenuna hadi unaogopa kuomba punguzo. Mwaka 1955 David Ogilvy aliwahi kusema, “Mteja siyo mjinga; mteja ni mke”. Mke anahitaji kupendwa; kubembelezwa; kupetipetiwa; kupewa raha. Ukimpa stress atakwenda kutafuta raha kwingine.


Umeweka namba za simu tukikupigia hupokei; kwa nini tusiwapigie wanaopokea? Umeweka namba za simu hazipatikani. Wewe ni mgonjwa. Yesu aliwapenda wateja wake hadi akawa tayari kuwafia. Je uko tayari kuwafia wateja wako? Au uko tayari kuwaua. Kuwaua kwa  chakula kilichoexpire sikuwaua? Hata anayeuza wali uliolala kila Jumapili anakwenda kanisani.


No one buys from silent sales people walisema wazungu. Hata Biblia inauliza, “Lakini watu watamwitaje yeye ambaye hawajamwamini? Na watamwaminije yeye ambaye hawajawahi kumsikia? Na watamsikiaje kama mtu hakuwahubiria? (Warumi 10:14). Maana ya mstari huu wa Bible ni kwamba watu wataaminije kitu hawajakisikia wala kukiona?


Tangaza biashara yako kwa lugha nzuri. Usitumie lugha yenye ukakasi na maudhi kama mtumishi mmoja aliyesema *Dunia Tulikuja Kunya tu!* Hahahahaa. Dunia hii inawatu wazito kuanzia kichwani hadi mdomoni. Mungu tuhurumie.  “Great marketing makes the customer feel smart” alisema Joe Chernov.


Kama una pesa nyingi kuliko akili wekeza kwenye matangaza; kama una akili nyingi kuliko pesa wekeza kwenye matangazo alisema Guy Kawasaki. Biashara yako ni moto; matangazo ni petrol.  Wenye akili ni wengi lakini wanaojulikana ni wachache. Hatuwezi kujua uwezo wako wa akili kwa kufaulu mitihani. Tutajua uwezo wako wa akili kwa kujitangaza.


Nimalizie kwa kusema natangaza ofa ya Ramadhani kuanzia dakika hii; utapata vitabu vitano kwa Sh 10,000; vitabu vyenyewe hivi hapa; Ukombozi wa Fikra; Maisha ni Kutafuta Siyo Kutafutana; Wasomi Huru Gerezani; Ukombozi wa Fikra za Mwafrika’ Viongozi Wanaoishi Baada ya Kufa. Vitabu ni softcopy, lipa kwa Mpesa 0753665484.


Ukitaka Hardcopy ni Sh 10,000 tu kwa kila nakala na tunapatikana nchi nzima kwa namba zifuatazo!


*Iringa*


0755100502


0753-690907


Au tembelea Citymax Booshop!


*Dodoma*


0755100503


0753 690 907


Au tembelea Citymax Booshop!


*Tabora* 


0765052507


*Tanga* 


0627186623


*Biharamulo*  


0753383461


*Mtwara* 


0786408811 na 0717408811


*Dar es Salaam* 


0745252670 na 0756094875


*Mbeya*  


0744241744


*Mbeya Mwanjelwa* 0763943695


*Kahama* 


0767872191 au


+255657948776


*Tunduma*


0685453333


0769634248


0656512333


*Katavi* 


0762255463


*Moshi na Arusha* 


0744 126 082


*Morogoro* 


0782144920


*Kahama* 


0755833533


*Dodoma mjini Mipango* 


0692983162


*Makambako*


0762282599


0674246969


Au tembelea  P. M Stationery and Book Shop Makambako Mizani


*Mwanza*


0754 977 848


Au tembelea Lavena supermarketi mwanza


*Mwanza mjini*


 0767949399 au +255652707919


*Mikumi Morogoro*


0757010979 


0715010979


*Singida na Katesh-Babati


 0789457475 


*Bei ni Sh 10,000 tu!


Kwa mlioko nje ya nchi tunatuma kwa DHL, piga namba 0753-690907


*Unataka softcopy?* Lipa Sh 5,000 kwa Mpesa 0753665484, jina Denis Mpagaze utumiwe kwa Whatsapp au email


Unataka uwakala? Piga 0753-690907. Faida ya kuwa wakala ni kwamba, tunakutangazia!


_*Tafuteni kwanza ukombozi wa fikra na mengine mtazidishiwa!*_

Jukwa La Fikra ni mwanga umulikao akili!