Unahitaji kujifunza ili kuboresha mahusiano yako na wengine. Unahitaji kujifunza ili kuboresha kazi yako. Ili kupata mbinu bora za kushindana na washindani wako na kuongeza thamani kwa wateja wako katika biashara, unahitaji kujifunza. Wewe mwenyewe binafsi ili ukue na kuendelea kuwa bora kila siku unahitaji kujifunza pia.

Ili uwe bora kila siku na usiachwe nyuma na dunia, unahitaji kujifunza kila siku rafiki yangu. Unahitaji kusoma vitabu, unahitaji kuuzulia semina, unahitaji kusoma makala kama hizi kupata maarifa kila siku, na kuna muda inabidi urudi darasani kabisa usome.

Kujifunza hakuishii chuo, kunaisha siku utakapotoka hapa duniani. Kadiri unavyojifunza kila siku utakuja kugundua kwamba hata kama unajua vitu vingi kiasi gani, lakini bado kuna vitu vingi utakuwa hujui.

Tafakari njema. Usiache kujifunza kila siku rafiki yangu.

Jukwaani ni mimi Dady Lutelemla >+255620306815