Bwana mmoja alikwenda kutembea ukweni kwake. Ilipofika usiku aliamka kwenda kujisaidia lakini kwa bahati mbaya taa zote zilikuwa zimezimwa. Wakati anapapasa ili kuwasha taa, alipamia vyombo vya chakula jikoni. Kipindi anajaribu kuviweka vizuri, mara taa ikawashwa na mama mkwe akamuona yule bwana ameshika vyombo na kumwambia, “Baba kama hukushiba ungesema.”
Mama mkwe alitumia hisia kujaji.
Hakujipa muda wa kufikiri. Shida ya hisia inakupa majibu ya haraka ambayo yanaweza kukuletea shida. Unadhani yule bwana aliendelea kukaa ukweni? Ndiyo yaleyale unaenda kutembea sehemu unaskia wanasema sisi humu hatujawahi kuibiwa kitu.
Kichwa kisipofanya kazi vizuri ya kufikiri utakuwa mtu wa kuchafua hali ya hewa kila siku.
Hisia ni matokeo ya kutojipa muda wa kuutafuta ukweli na hivyo kuangukia kwenye mtego wa harakaharaka haina baraka. Wengi wameumia kwa sababu ya hisia.
Siku moja ndoa inafungwa kanisani, Mchungaji akauliza, “Yeyote mwenye pingamizi la ndoa hii kufungwa aje mbele.”
Kibabu kimoja kikasimama na kwenda mbele. Bi harusi kuona hivyo akaanguka na kuzimia! Mchungaji, akakiuliza kibabu,
“Tuambie babu pingamizi lako!” Kibabu kikajibu,
“Nimeamua kuja mbele, kule nyuma sisikii vizuri!” Hisia zilimzimisha Bi harusi. Tuwe na subira katika kuungoja ukweli. Ukweli una tabia ya kuchelewa lakini lazima ufike.
Kama unafaidika na Jukwaa la Fikra, jaribu kuwaalika na marafiki zako ili mfaidike wote, maana waswahili husema "kizuri kula na wenzako"
Kwa ushauri niandikie email dadylutelemla@gmail.com au WhatsApp namba 0620306815
Mimi ni Dady Lutelemla mjenzi wa Fikra Jukwaani.
0 Comments