Mwanangu mpendwa, hii ni yako. Katika malezi ya mtoto kuna mambo mengi sana.
Umekua katika mikono yetu salama umesoma mpaka hapo ulipoishia, tulikujali sana ili hali tukijua wewe ni wetu, hatukuruhusu upate malezi tofauti na yetu, hatukukupeleka kwa babu au bibi yako.
Tulijibana ili kuhakikisha unapata kila ulichohitaji kutoka kwetu wazazi wako. Hatukuruhusu hata kuujua udhaifu wetu katika malezi yetu kwako.
Tulipambana ili nawe utimize ndoto zako.
Sasa mwanangu umekua, una maisha yako huko mjini, ni yapata miaka kadhaa sasa ukiwa unapambana na maisha yako.
Umezaa na mwanao kumleta huku kwetu kijijini ili tumlee sisi wazazi wako.
Uzazi wako uko wapi mwanangu? Mapenzi yako yapo wapi mwanangu?
Waswahili wanasema " maji ukiyavulia nguo Sharti uyaoge" uliamua kuzaa bila kusubiri uolewe au uoe, hayo ni maji yako yaoge, oga maji yako mwanangu ili mwanao ajue tupo na shujaa kama ambavyo unatuposti Sisi wakati wa siku ya wanawake au wanaume.
Tengeneza ushujaa kwa mwanao mwanangu, ishi naye, mpe malezi yote wewe mwenyewe, jibane kamwe asione madhaifu yako.
Huu ni ujumbe wako mwanangu niliouacha hapa katika Jukwaa la Fikra.
Kama umepoteza mawasiliano yangu nitafute kwa WhatsApp namba 0620306815 utanipata.
Asante.
0 Comments