Kila dakika unayokasirika unapoteza dakika 60 za furaha. Hasira ni hisia zenye maumivu ya ndani! Ni sawa na kujiadhibu kwa kosa la mwingine. 

Jinsi unavyozidi kukaa na hasira ndivyo unavyozidi kuumia.Ni sawa na kushika kaa la moto! Ni wajinga tu ndio hukaa na hasira kwa muda mrefu alisema Albert Einstein. 

Lakini hata Biblia inatuasa tusikae na hasira kutwa nzima (Efe 4:26). Hakikisha jua lisizame bado umezila. 

Hasira ni asidi inayoweza kusababisha madhara makubwa kwenye chombo kinachoitunza kuliko chombo kilichoileta! 

Hatuwezi kujizuia kukasirika, lakini tunaweza kudhibiti matendo yetu wakati wa hasira. Kuna mtu anawahi kukasirika na kuwahi kupoa. Huyu hana shida! Mwingine anawahi kukasirika na kuchelewa kupoa. Huyu yuko kwenye hatari kubwa. 

Hasira siyo kitu kibaya kwa sababu kukasirika ni sehemu ya utu; kuzitawala hasira ndio kunafanya mtu awe mtu; kushindwa kuzitawala ndio hufanya mtu awe kitu, au tuseme mtu awe kituko! 

Endelea kunisapoti kwa kufuatilia jukwaa la Fikra kila mara.

Nitafute kwa WhatsApp namba +255620306815, kwa ushauri na maoni yako maana wewe ndiyo mwenye jukwaa.

Dady Lutelemla ndiyo jina langu.