*Nukuu 16 kuhusu ubahili kutoka kwa Bahili wa Taifa: Anaitwa Chaula!*
1. Ubahili ni hali ya kuwa mwepesi kupokea na kuwa mgumu kutoa.
2. Ubahili ni hali ya kuwa na moyo mgumu kutoa.
3.Kanuni ya kanisani inasema NI HERI KUTOA KULIKO KUPOKEA; kanuni ya uchumi kanuni yetu inasema NI HERI KUPOKEA KULIKO KUTOA.
4. Wachaga wengi ni wafanyabiashara wakubwa kwa sababu ya ubahili wao.
5. Usitoe ili kumfurahisha mtu, uchumi siyo burudani; uchumi ni vita.
6. Siyo kila anayekuomba pesa lazima umpe pesa. Mwingine unatakiwa umnyime pesa lakini umpe maarifa ya kupata pesa.
7. Fedha haitolewi hovyo hovyo na siyo dhambi kumnyima mtu anayeomba fedha.
8. Huwezi kumaliza shida za kila mtu, ukiwa unampa hela na Mali kila mwenye shida utafilisika bure na uliowasaidia hawana uwezo wa kukusaidia tena.
9. Epuka kutengeneza kundi la watu wengi kukutegemea bila sababu za msingi.
10. Huwezi kuwa tajiri kama unategemewa na watu wengi na unatoa hela hovyo kwa ndugu, jamaa na marafiki zako bila hesabu.
11. Wakati mwingine Mungu anamleta mtu kwako siyo umpe hela ila umpe mbinu ya kupata hela.
12. Kwa wenye ndoa hata kama mmepeana vingine lakini hela mnaweza kunyimana kwa kuheshimu bajeti.
13. Hela haina mchezo ndiyo maana wengi wameishia kuishi maisha ya kimasikini.
14. Fedha ya mtu na iheshimiwe na watu wote. Siyo mwenzenu amepata fedha kidogo tuu basi ukoo mzima mhamie kwake na matatizo ya ukoo mzima Hadi ya majirani abebeshwe yote.
15. IIi uwe tajiri lazima uwe bahili kweli kweli na roho ngumu kwenye hela.
16. Ukipata fedha tulia na uiheshimu na uwe na nidhamu kwenye kutumia kwa kuwa ukifilisika siyo rahisi kurudi kwenye mstali kirahisi.
+255620306815 utanipata tuyajenge
0 Comments