Kweli ya 1

Usijaribu kukata tamaa kwa sababu Mungu anaweza kubadili kila kitu katika maisha yako kwa dakika sifuri! Mungu ni fundi. Namkubali sanaaa! 

Kweli ya 2

Ukiwa darasani jibu la 2x3 ni sawa na jibu la 3x2. Yaani 6. Lakini ukiingia mtaani majibu ni tofauti. Kama haumini subiri Daktari akuandikie dozi ya 3x2 kutwa halafu we meza 2x3 halafu sikilizia! Ukifa ni ubishi wako. 

Hata ushirikiano wakati wa mtihani darasani ni wizi na wakati mtaani maisha bila ushirikiano hayaendi. 

Kweli ya 3

Kundi la Waafrika kwenda Ulaya wanaitwa Wakimbizi lakini kundi la Wazungu kuja Afrika wanaitwa Watalii! 

Kundi la Waafrika wakionekana maporini ni majangiri lakini, kundi la Wazungu wakionekana maporini ni watafiti! Hapa napo kuna kula na kuliwa. Analiwa mjinga, anakula mjanja! 

Kweli ya 4

Ukiwapatia chakula maskini unaitwa msamaria mwema, ukiuliza chanzo cha umaskini wao unaitwa mchochezi!

Nicheki kwa namba yangu 0620306815 tuzijue kweli nyingi zaidi.