Kaishi Naye Kwa Akili
Kijana Wangu; Ndoa hujengwa kwa mawe ya upendo na sakafu ya utii! Kupenda ni jukumu la mwanaume. Kutii ni jukumu la mwanamke.
Ukimpenda atakutii. Ukimchukia atakudharau.
Kumpenda mwanamke ni kumhudumia.
Hatupendi kwa mabusu na tabasamu.
Tunapenda kwa fedha na dhahabu! Mabusu na tabasamu ni vionjo vya mapenzi, siyo mapenzi.
Kijana Wangu; Ukishindwa kumhudumia mwanamke atajihudumia. Akijihudumia atakudharau. Hujawahi kusikia wanasema siwezi kukaa na mwanaume asiyenihudumia?
Na hii siyo kwa wanawake tu. Ni sehemu zote. Duniani hajawahi kuheshimiwa mtu.
Yanaheshimiwa matokeo ya mtu.
Huna cheo nani atakutii? Huna umaarufu nani atakutii? Huna pesa nani atakutii? Huna pesa hata mbwa wako anaweza kukuuma!
Tuutafute kwanza ukombozi wa fikra ndani ya Jukwaa la Fikra na yote tutafunguliwa.
Nitafute kwa WhatsApp namba 0620306815 tupeane michongo.
0 Comments