Dady Lutelemla na Denis Mpagaze
______________________________________
Akili yako ni sawa na kisu kikali ambacho usipokitumia vizuri kitatumika kukuchinja! Kuna watu akili zao zimewapeleka jela, wengine kaburini, wengine zimewaambukiza magonjwa, itoshe kusema tu watu wengi wamechinjwa na akili zao wenyewe na wengine wanaendelea kuteseka kwa sababu ya akili zao. Ukitumia akili vizuri inalipa, ukitumia vibaya inaliza.
Sasa sikiliza kuna siri nyingi katika matumizi ya akili.
Moja ya siri hiyo ni uwezo wa kukuunganisha na nguvu ya asili. Kila mtu ameishawahi kuingiwa na nguvu za asili kwa kujua au kutokojua na kuishia kusema ni Mungu tu! Utasikia nimepona kwenye ile ajali? Ni Mungu tu! Ukimuuliza ameponaje anasema hata mimi nashangaa.
Lazima ushangae kwa sababu hiyo ni nguvu ya asili ambayo ikiingia ndani mwako lazima ufanye mambo makubwa na ya kushangaza.
Likipigwa bomu unaweza kujikuta juu ya kabati la nguo umekaa. Ulifikaje huko? Nguvu ya asili.
Nguvu za asili hutokea pale unapokutana na jambo la kutisha au kufurahisha sana. Mgonjwa mahututi akisikia habari za mshahara umetoka anapona ghafla. Mlemavu anayetumia magongo timu yake ikifunga utamkuta yuko uwanjani akishangilia magongo kaacha kwenye siti.
Nguvu ya asili. Nguvu hiyo ikitoka anapata shughuli ya kutafuta magongo arudi!
Vumbuzi kubwa za kustaajabisha zimetokana na nguvu ya asili.
Ukiweza kuinasa nguvu hii unaweza kuufanyisha mwili wako kitu chochote ukitakacho na kikafanyika. Unashauriwa unapokuwa na changamoto yoyote ile, iruhusu akili yako kuwasiliana na nguvu za asili uone utakavyopata majibu kiulaini.
Hakikisha unakwenda kulala na wazo moja tu la changamoto hiyo ili iwe rahisi kukupatia jibu.
Swali ni je unaweza kuwaza kitu kimoja tu akilini bila kuingiliwa na mawazo mengine kibao? Thubutu! Changamoto za dunia ndo husababisha akili zetu kuwa busy muda na mawazo ya kila aina tena muda wote.
Uko zako kazini lakini akili inawaza ada za watoto; kodi ya nyumba, inawaza biti la mchepuko, ukali wa bosi wako na mwisho wa siku ufanisi wako kuwa poor.
Watu wengine wamekuwa vichaa kwa sababu ya mlundikano wa mawazo katika akili zao. Hizo tunaita takataka ndani ya akili!
Sasa sikiliza. Ipo njia rahisi sana ya kuondoa hizo takataka akilini mwako. Inaitwa meditation, yaani tahajudi kwa Kiswahili kigumu. Wanafanya sana wazungu, waarabu na wahindi. Hao jamaa akili ikizidiwa wanameditate, sisi akili ikizidiwa tunalewa.
Meditation ni nini basi? Meditation ni zoezi la kuondoa mawazo yote akilini na kubaki na wazo moja tu au ukiwezekana ubaki bila wazo.
Yaani kama unataka kujenga nyumba, waza nyumba tu, unataka kulima matikiti waza matikiti tu. Ukifanya meditataion kwa dakika 15, siku nzima itakusaidia kuwaza jambo hilo tu na kulifanya kwa uhakika! Kumbe ni vizuri kufanya hiyo kitu kila siku. Sasa mfano unatafuta kodi ya nyumba na umekosa kabisa, fanya meditation yako dk 15, kisha kalale zako, huko usingizini lazima upate majibu maana utakutana na nguvu ya asili.
Kumbe meditation inasaidia kuipumzisha akili, kutibu matatizo ya kisaikolojia, kuratibu msukumo wa damu pamoja na usafirishwaji wa damu mwilini kwa sababu akili ambayo ndo kiongozi wa yote haitakuwa busy tena.
Ondoa takataka akilini mwako kwa kufanya meditation kila siku. Meditation inafanya kwa dakika kuanzia tato hadi 15. Unaifanyaje basi? Tafuta sehemu isiyokuwa na kelele hata kidogo, unaweza kwenda porini au ukasubiri usiku wa manane; kaa chini au kwenye kiti au sehemu yoyote utakayofeel confortable then anza kumediatate, waza kitu komoja tu, hakikisha akili haihami, ni kazi ngumu lakini ukifanya mara kwa mara utazoea na utaona maajabu yake.
Ziko meditation za aina nyingi, lakini leo tufanye meditation ya kufuta takataka usizozipenda akilini mwako, yaani tabia mbaya au maneno mabaya uliyonenewa. Weka mshumaa wako mbele yako kwenye stuli au kitu chochote ili mradi uwe usawa wa macho yako. Uwashe na uanze kuuangalia kwa kuukazia macho bila kupepesa kope. Fanya hivyo kwa dakika hadi 30.
Anza kuchoma mambo ambayo uliambiwa huwezi. Mfano, uliambiwa huna akili. Chukua hili neno lililokaa akilini lichome kwenye moto huu wa mshumaa nakwambia halitakuja tena. Kila ukitaja jambo hilo baya utaona moto wa mshumaa ukiongezeka au ukibadilika rangi. Tahadhari wakati unachoma, usije kachoma mambo mazuri.
Fanya zoezi hilo la kuchoma balaa halafu kesho uje hapa uniambie uliona nini. Zoezi la meditation tulifanyeni kwa miezi sita! Emily Fletcher anasema mafanikio makubwa hayaletwi kwa kufanya kazi kwa bidii tu bali kwa kusafisha akili. Anasema alivyoanza kazi ya uigizaji aliona kama hatoboi hivyo akaomba ushauri kwa rafiki yake akaambiwa jibu ni meditation. Akasafiri hadi India kujifunza meditation kwa miaka mitatu. Alivyorudi akatoboa. Fanya meditation kuwa sehemu ya maisha yako.
Unaweza kujisomea vitabu vyote hivi kumi kwa kuchangia bando tu Mpesa 0753665484.
1. Be the Change_ How Meditation Can Transform You and the World
2. How to Meditate_ A Practical Guide to Making Friends with Your Mind
3. How To Meditate_ A Step-by-Step Guide to the Art and Science of Meditation
4. How to Teach Meditation to Children_ Help Kids Deal with Shyness and Anxiety and Be More Focused, Creative and Self-confident
5. Life Is Meditation - Meditation Is Life
6. Meditation and Its Methods
7. Meditations
8. Meditations to Heal Your Life
9. Mindfulness Meditation (For Everyday Life)
10. The Beginner's Book of Meditation_ A Practical Guide to Meditation and Breathing Techniques
11. The Daily Stoic_ 366 Meditations on Wisdom, Perseverance, and the Art of Living
12. The Heart of Meditation
13. The Power Is Within You
0 Comments