Mwanangu umekua, unaweza kufanya kila jambo uliwezalo kwa mikono yako. Katika ufanyaji wako wa kazi jitahidi sana kuwa makini kwa sababu binadamu hao hao ambao watakupa michongo ndiyo hao hao ambao wanaweza kukuharibia michongo yako pindi mambo yako yatakapoonekana yamekunyookea. 
 Katika juhudi zako zote mwanangu jitahidi sana ufiche mambo makuu mawili kwenye kila unachokianya 

 *Jambo la kwanza: Ficha sana udhaifu wako, kuficha udhaifu wako kutakufanya usiwe mwepesi wa kufikika kirahis kwa mambo yasiyo ya msingi, mwanangu kumbuka kuwa mapungufu yako ndiyo hutumika kuinua mengine, kama upo katika fursa fulani jitahidi sana kuficha udhaifu wako ili kutowapa mwanya watu wengine watumie upenyo huo kuinuka. 

 *Jambo la pili ni Uimara wako, uimara wako ndiyo mafanikio yako, ndiyo maendeleo yako, mwanangu katika kila nyanja unayoifanya jitahidi mtu asijue uimara wako juu ya jambo hilo. Usioneshe kuwa unaweza je kufanya jambo fulani kwa kiasi gani kwa sababu kupitia uimara wako watu hutumia ili kuweza kukuangisha, kumbuka hata Samson aliangushwa pale tu aliposema kwa mpenzi wake Delira kuwa nguvu zake zipo katika nywele, hivyo aliponyolewe tu nguvu zake zikaisha na akapigwa kiurahisi. 
 Hapa mwanangu najaribu tu kukukumbusha kuwa katika kila jambo unalolifanya jaribu kuwa na kiasi. Kuwa na kiasi ya maneno na hata matendo. 

 Mwanangu nimekupa ujumbe huu katika Jukwaa La Fikra kwa kuwa utawaambia na vijana wenzako juu ya mambo haya mawili niliyokuambia, kamwe usiwe mchoyo wa elimu na maarifa uyapatayo humu Jukwaani. 

 Napatikana kwa namba ya WhatsApp +255620306815 au piga kawaida +255654836144 utanipata tutaongea nawe ili kuweza kuelekezana zaidi. 

 Ni mimi injinia wako katika Jukwaa la fikra Dady Lutelemla