Mahusiano ndiyo maisha, mahusiano ndiyo mafanikio, mahusiano ndiyo maendeleo ya kila eneo. Ukiwa na mahusiano mzuri na imara utafika mbali.

Leo kupitia Jukwaa la fikra ningependa nigusie kuhusu kutunza mahusiano haya ya aina tano katika maisha yako.

1: Mahusiano na Muumba.

>Mahusiano na Mungu ni kitu kimoja kikubwa sana katika kujenga au kubomoa jambo fulani, ukijenga mahusiano imara na Mungu hakika utafika mbali sana, Mungu amejidhihirisha wazi kupitia vitabu vyake, hivyo hakikisha unatengeneza uhusiano mzuri na yeye ili mambo yako yaende. Amini kwa imani kubwa na weka juhudi binafsi kwa kila unachokifanya kuwa yupo msimamizi wako hivyo kuwa makini sana kuvunja mkataba wako wewe na msimamizi huyo. Tumia gharama kuujenga uhusiano huu.

2: Mahusiano ya ndoa/mapenzi.

>Katika sekta hii ya mahusiano kumekuwa na changamoto kubwa sana, maisha ya watu wengi yamefeli, uchumi wa watu wengi umedumaa, afya za watu wengi zimesinyaa, na matokeo yake watu wamekata tamaa kabisa.

Kitu kikubwa nataka nikwambie ambacho haujawahi kuambiwa sehemu yoyote ni kwamba mahusiano haya ndiyo yamefanya dunia ijae, ndiyo yamefanya na wewe unayeaoma Jukwaa hili uwepo. Kitu pekee cha kukuasa ni kwamba katika mahusiano ya ndoa watu wanaingia wakiwa kila moja na mapungufu yake, nia ya kuungana ni kufidia nguvu zako kwa mapungufu ya mwenzako. 

Tumia gharama yoyote kuhakikisha unayajenga mahusiano haya. 

3: Mahusiano na kazi.

>Mungu alipoumba ulimwenngu kitu cha kwanza kumwambia binadamu ni afanya kazi, haijarishi unafanya kazi gani, tengeneza mahusiano mazuri na kazi.

Unatengeneza mahusiano mazuri na kazi kwa kufanya kazi kwa bidii na akili, kufanya kazi kwa moyo wako, kuipenda kazi na kuweka ushirika mzuri na watu unaofanya nao kazi, kama ni mfanyabiashara tengeneza mahusiano mazuri na wateja wako, kama umeajiliwa hakikisha unaweka uwiano sawa baina ya mwajiri wako na wafanyakazi wenzako.

Tumia gharama yoyote kuhakikisha unakuwa katika msitari mzuri na kazi yako.

4:Mahusiano na afya yako.

>Watu wamekuwa wakiweka vipaumbele vingi katika maisha lakini suala la afya binafsi limekuwa changamoto,. Mgonjwa mengi yamezalishwa kwa mtu kushindwa kuwa na mahusiano mazuri na afya yake binafsi,

Unataka kuwa na afya imara, tengeneza utaratibu bora wa namna unavyoongea, namna unavyokula, namna unavyokabiliana na changamoto za maisha. Watu wengi wamejitia matatani kwa namna ya kuzungumzia kwao, wamekosa amani ya nafsi na kujiua kwa kushindwa kukabiliana na changamoto za maisha na hata mfumo wa ulaji ambao ndio limekuwa chanzo cha afya za watu wengi kuzoroteka. 

Kama utumiavyo gharama zingine, tumia pia gharama kubwa kuhakikisha hauharibu afya yako mwenyewe. 

5: Mahusiano na wewe.

>Kitu cha mwisho kabisa ni unatumia muda gani kujenga uhusiano baina yako na wewe, ni ukweli usiopingika kabisa kuwa maongezi unayozungumza wewe na wewe ndiyo maisha halisi ya wewe kwa muda husika, nafsi na moyo wako daima huzungumza mambo yaliyo ya kweli kila unapojaribu  kukaa navyo mahali.

Kujichanganya, kuomba ushauri kwa watu ni jambo la maana ila hakuna jambo la busara zaidi ya kukaa peke yako na kuongea na wewe.

Tenga muda wa kukaa na wewe mwenyewe na hakikisha unautumia vyema, majibu utakayopata utaniambia kwa WhatsApp namba +255620306815 au utapiga kwa namba +255654836144 unipe ushuhuda.

Ni injinia wako katika Jukwaa La Fikra Dady Lutelemla Jilasa.