Tumaini langu kubwa ni kuwa unaendelea vizuri na una shauku kubwa ya kutaka kujua Leo kuna nini jukwaani.
Leo nimekuja kukutia hamasa, nimekuja kukata minyororo ya aibu, minyororo ya kutoaminiwa, minyororo ya majuto. 

Nilishawahi kuwa binadamu wa ajabu kabisa. 
Nilishawahi kuwa binadamu mpenda kamali,. 
Nilishawahi kuwa binadamu jambazi,. 
Nilishawahi kuwa binadamu mchoyo,. 
Nilishawahi kuwa binadamu  mshinda vijiweni,. 
Nilishawahi kuwa binadamu mpenda uzinzi,. 

Kuna wakati mtu unajiuliza kuwa unatokaje kwenye minyororo hii ya vifungo vya aibu na kutoaminiwa? 

Unawaza utajikwamua vipi na wimbi hili la kutopewa nafasi. Jambo kubwa hapa ni kuanza kubadilika, anza mazoezi ya taratibu ya kubadilisha mfumo wako wa maisha. 

Hatuna Garantii na dunia, hivyo unavyopata mwanya wa kuwaza kuwa unachokifanya siyo sahihi katika uso wa dunia, anza mara moja kutafuta namna sahihi ya kukiacha. 

Tuzo ya heahima zaidi Duniani ya Nobel Peace Prize ilianzishwa na Bwana Nobel, ambaye alikuwa mtu wa ajabu zaidi kuwahi kutokea katika karne. 

Unajua ilikuwaje, jamaa aliamka na kwenda sehemu wanapouza magazeti na akakuta chapisho lililoandikwa "DUNIA SASA IPO HURU, LILE JAMBAZI SUGU LIMEKUFA". Aliyekuwa amekufa ni mtu mwingine anayefanana naye, hivyo magazeti yalichapishwa kimakosa! 

Bwana Nobel baada ya kuona hivyo ikawa mwisho wa uovu wake na akabuni namna ya kutoa heshima kwa wapigania uhuru, na sasa Tuzo yake ndiyo Tuzo ya heshima zaidi Duniani. 

Usisubiri mpaka uone watu wanakuongeleaje, anza sasa, Lete mabadiliko yako kuanzia katika familia yako, mpaka katika ngazi ya nchi na Dunia. 

Napatikana kwa WhatsApp namba +255620306815 au piga simu kwa namba +255654836144. 

Wako Dady Lutelemla Jilasa.