Habari za wakati huu mpenzi msomaji na mfuatiliaji wa Jukwaa la fikra, imani yangu umzima wa afya njema kabisa. Karibu tena jukwaani tuweze kuangazia yale yanayotuhusu.

Leo nitakuwa tofauti kidogo kwa sababu na mimi huenda nikaingia kwenye list ya siyo ajabu kabisa,. Twende sawa hapa chini.

Katika hali ya kawaida binadamu hudharau sana kile kitu kilicho cha kawaida na kuvipa thamani vile vilivyo juu yake au vieleavyo pekee.

Ukweli ni kwamba siyo ajabu kabisa kufundishwa na mtu aliyefeli mtihani na wewe ukafaulu, siyo ajabu hata kidogo kwa sababu hata ukiangalia mfumo wetu wa elimu unamruhusu mtu aliyefeli kwenda kusomea ualimu ili afundishe watu wafaulu kwenda kuwa maprofesa na maPhD, hili liko wazi kabisa na halihitaji tochi.

Hivyo siyo ajabu kabisa kikubwa tambua tu ni kitu gani unakitaka kutoka kwake.


Siyo ajabu kabisa kumsikiliza maskini akifundisha mbinu za kufanikiwa, siyo ajabu hata kidogo, ajabu ni pale unapompotezea na kisha wote mkabaki chini kitu ambacho ungetumia muda kumsikiliza na ukafanyia kazi yale aliyoyasema ungepanda juu kimaisha na ukaja ukamuinua pia. Kitu pekee ambacho nataka nikwambie hapa jukwaani ni kwamba hakuna asiyejua mbinu za kivita, kinachogharimu ni vifaa vya kivita. Kuwa maskini haimaanishi haujui mbinu za kufanikiwa, wakati mwingine huwa ni ukosefu wa vyanzo tu.

Usione ajabu kabisa kumsikiliza maskini, tena tuna mbinu nyingi sana, kikubwa wewe tambua tu unataka nini kutoka kwetu.


Siyo ajabu kabisa kuhamasishwa na aliyehamasishwa kwani watoa hamasa wengi ni wale ambao wamehamasishwa na bado hawajahamasika, hivyo wakihamasika wenyewe hawatayasema yale yaliyowafanya wahamasike,, siyo ajabu kabisa kuwasikiliza hawa watu,, wana nondo za kutosha. Nani anaamini kuwa Bill Gates alikuwa maskini? Unaamini vipi? Kifupi nataka nikwambie ukifanikiwa upo huru kutengeneza historia ya maisha yako,, tena ili historia ya mafanikio yako ilete maana ni lazima iwe ya ajabu,, lazima uweke vipengele vya kusota, vipengele vya kukataliwa, kitengwa, na hata kuwa mtu wa ajabu tu.

Ushawahi kusikia historia ya mchungaji wako au imamu wako? Nenda kawasikilize uone kama katika historia zao hawatakwambia kuwa bila Mungu wangekuwa majambazi majitu ya ajabu.

Tumia muda kuwaaikiliza tu watu hawa haina ajabu kabisa, ila tambua kitu unachokitafuta kutoka kwao.


Siyo ajabu pia kumuona mtu aliyeachika au kuachwa akifundisha namna bora ya kudumisha ndoa, siyo ajabu hata kidogo, ajabu kubwa inapokuja ni kwamba unamsikiliza kwa namna ya kupata umbeya, watu hawa wanauzoefu wa kutosha juu makosa yaliyo ndani ya mahusiano, wana uzoefu wa hali ya juu kuelezea madhaifu ya mtu aliyekuwaga nae, tumia muda huo kumsikiliza akimwagika ili uchukue tahadhali mapema, tatizo lako ukishamsikiliza na wewe unatumia mwanya huo kwenda kwa mtu aliyemuacha ili nawe uuone upuuzi alioufanya kwa rafiki yako. Sijui hii imakaaje, unamchukua mpenzi wa rafiki yako aliyemuacha?

Tumia muda kumsikiliza ili ujijenge vyema na kwa ubora wa hali ya juu.


Mwisho siyo ajabu kuwa tofauti na wengine, wakati mwingine kufanikiwa siyo lazima ufanye kile wenzako wanakifanya, kufanikiwa siyo lazima ufate nyayo tu kama tulivyoambiwa na watu wengi, kwani ukianzisha nyayo zako hautafika?

Unapokuwa unaishi Usione ajabu kuwa mtu wa tofauti, kuwa tofauti utasemwa, utatengwa, na kunyoshewa vidole ila tambua kuwa unapokuwa tofauti ndiyo unajenga au kuandaa historia ya maisha yako iliyo mbaya na yakusisimua watu na kujifunza pia, kwa kifupi unaandaa mafanikio yako. Ni ajabu kubwa mno kufanya kama wafanyavyo na wote mkabaki vile vile mnatazamana na nani wakupuliza kipenga. Uwanjani kungekuwa wote wapuliza vipenga tusingeinjoy mpira safiii, wangekuwa wote mabeki tusingeona magoli murua kabisa,

Utofauti unatengeneza radha ya maisha.

Kunibariki pia na mimi nisionekane wa ajabu inaruhusiwa. Nicheki WhatsApp kwa namba +255620306815 au nipigie kwa namba +255654836144.

Ni mwanagenzi Jukwaani Dady Lutelemla Jilasa.


Cheers, na share pia! Love you all!