Kwenye maisha kuna vitu vingi sana tunaviona vya kawaida sana pale tunapokuwa navyo karibu au tunavimiliki. Lakini ni ukweli usiopingika kuwa vitu hivyo huwa vinaleta maafa makubwa zaidi vinapokuwa vimetoweka tena katika uso wa karibu.

Ni kawaida sana kwa mtu kuona kazi aliyonayo kuiona ya kawaida sana lakini siku ikipotea ndiyo unaweza kuona thamani na mchango wake mkubwa katika maisha ya kila siku, Umeajiriwa sehemu, unaingia ofisini bila bugudha ya aina yoyote, haupigi hodi, hautishwi na mlinzi wala hauulizwi kwa namna yoyote.

Jaribu sana kutunza kazi hiyo kwa sababu siku ukiondolewa ndiyo utaona thamani yake, hautakuwa na uwezo wa kukanyaga pale bila ridhaa, bila ruhusa na ahadi maalum, itakuwa ngumu mnoo.

Tunza sana kazi hiyo kwa sababu yaweza ikawa ndiyo furuha yako kwa sasa. Kumbuka kuna watu wanatamani sana kuwa na kazi kama yako, wanatamani kuingia hapo getini lakini wanaishia kutukanwa na mlinzi wenu, tunza sana hiyo furaha.

Yawezekana una mke au mme, unapata furaha kila unapoihitaji, hauombi ruhusa wala hauhitaji gharama kubwa sana, unachokitaka unakipata kwa muda muafaka, usimuone wa kawaida ukamdharau, ukamshusha thamani yake kwa kuwa anaingilika kiurahisi, kuna wakati utamkosa ndiyo utajua kuwa hata kope zina umuhimu mkubwa katika utendaji kazi wa macho.

Kuna mengi lakini naomba nishuke Jukwaani ili nisikuchoshe maana nimeambiwa hata hauna mood ya kusoma tena.

Basi nicheki kwa WhatsApp namba +255620306815 au nipige kwa namba +255654836144.

Dady Lutelemla, mtunzi Jukwaani.